11 Aprili 2025 - 18:32
Source: Parstoday
Jenerali Qa'ani: Marekani, Israel 'ni dhaifu kivitendo' mbele ya Iran na Muqawama

Kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kislamu nchini Iran amesema kuwa licha ya bwabwaja zao, Marekani na Israel "hazina nguvu kivitendo" dhidi ya Iran na makundi ya Muqawama.

Brigedia Jenerali Esmail Qa'ani amesema kuwa Marekani na Israel haziwezi hata kuelewa kwa nini makombora yetu yanalenga kwa usahihi shaba zao.

Mwezi Aprili na Oktoba mwaka jana Iran ilipiga kambi na vituo vya kijeshi na ujasusi vya Israel kwa kutumia makombora ya kadhaa. Maafisa wa Iran walisema kuwa hiyo ilikuwa sehemu ndogo tu ya nguvu na uwezo wa nchi katika kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wakati, wataalamu wa kijeshi wa nchi za Magharibi wakionya kwamba mashambulizi ya baadaye yanaweza kuwa magumu zaidi na kutumiwa idadi kubwa zaidi ya makombora, Kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) wiki iliyopita kilizindua mji mkubwa wa kombora wa chini ya ardhi. 

Mjii huo umezinduliwa baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kutishia kuwa ataishambulia Iran iwapo haitatii matakwa ya Marekani. 

Brigedia Jenerali Qa'ani alisisitiza jana umuhimu wa kujitegemea na uzalishaji wa ndani na kuyapongeza makundi ya Muqawama katika kanda hii kwa kuendeleza mapambano na kusimama imara kwa suhula chache dhidi ya zana za kivita za kisasa za adui.

Meja Jenerali Mohammad Bagheri Mkuu wa Majeshi ya Iran pia amesema kuwa kasi ambayo Jamhuri ya Kiislamu inakuza nguvu zake za ulinzi ni ya kubwa zaidi kuliko kasi ya kupona maadui.

342/

Your Comment

You are replying to: .
captcha